Chimbuko
Wilaya ya Rorya ilianza rasmi tarehe 01/07/2007 baada ya kugawanywa kutoka Wilaya ya Tarime. Kabla ya hapo Wilaya hii ilikuwa jimbo la uchaguzi la Rorya. Wilaya ipo kaskazini mwa Tanzania kati ya latitude 1o .00″ - 1 o 4.5″ Kusini mwa mstari wa Ikweta na Longitude 33o. 30″ - 35o.00″ Mashariki mwa mstari wa Meridiani. Wilaya inapakana na nchi ya Kenya Kwa upande wa kaskazini, Wilaya ya Tarime upande wa Mashariki. Wilaya za Butiama na Musoma kwa upande wa kusini na Nchi ya Uganda upande wa Magharibi.
Wilaya ya Rorya ina jumla ya Tarafa 4, Kata 26, Vijiji 87 na Vitongoji 506 na kaya 60,510 ikiwa Kata 24 katika Halmashauri ya Wilaya na Vijiji 87 na Mamlaka ya Mji Mdogo Shirati in Kata 2 na vitongoji 9.
Kwa mujibu wa matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Halmashauri ya Wilaya ilikuwa na wakazi 265,241 ambapo kati ya hao wanaume wlikuwa 126,247 (47%) na wanawake walikuwa 138,994 (53%); na kwa wa wastani wa ongezeko la watu (Population growth Rate) la asilimia 2.8, Wilaya ya Rorya inakadiriwa kuwa na wakazi 302,552 kwa mwaka 2017. Kati ya hao wanaume 144,006 na wanawake in 158,546 Kutokana na idadi hii ya wakazi, inakadiriwa msongamano wa watu kwa kilometa moja ya mraba kuwa ni 125.
Ukubwa wa Eneo
Wilaya ina ukubwa wa kilomita za mraba 9,345.496, ikiwa eneo la maji (Ziwa Victoria) ni kilomita za mraba 7,252 sawa na 77.6% ya eneo lote la Wilaya. Eneo la nchi kavu ni kilomita za mraba 2,093.496 sawa na 22.4% la eneo la Wilaya.
Watu wa Rorya
Wakazi wa Wilaya ya Rorya ni mchanganyiko wa makabila ya Waluo na Asili ya Wakurya(waliomeguka na kugawa makabila madogomadogo yapatayo sita).
Shughuli za Kiuchumi
Uchumi wa Wilaya ya Rorya unategemea hasa shughuli za kilimo, ufugaji na uvuvi. Aidha Mazao makuu yanayolimwa Wilayani ni Mahindi, Mihogo, Migomba, Mtama, Ulezi, Viazi vitamu, Maharage na mazao ya Biashara ni kahawa, Pamba, Ufuta na alizeti. Shughuli kuu za kiuchumi za wakazi wa Wilaya ya Rorya ni ;
Hali ya Hewa
Halmashauri ya Wilaya ya Rorya ipo katika mwinuko wa mita 800 hadi 1,200 juu ya usawa wa Bahari. Mtazamo wa ardhi ya Halmashauri ni rasi, ghuba, miteremko, tambarare, mawe yaliyojitokeza na mito inayomwaga/peleka maji katika ziwa Victoria. Kiasi cha mvua na hali ya hewa inatofautiana kutokana na umbile la ardhi eneo kwa eneo na mvuto wa ziwa. Kiasi cha mvua kwa mwaka ni kati ya mm 700 hadi 1200 kwa mvua inayonyesha misimu miwili.
Mvua za msimu wa vuli huanza mwezi Oktoba hadi Desemba na mvua za masika huanza mwezi Machi hadi Juni. Hali ya hewa ni ya joto la kadri, lenye vipimo vya nyuzi joto kati ya nyuzi 140C hadi 300C.
INGRI JUU - RORYA
Sanduku la Posta: 250 TARIME
Simu ya Mezani: 0282985583
Simu ya Mkononi :
Barua Pepe za Watumishi: mkurugenzi@roryadc.go.tz
Haki Zote Zimehifadhiwa